10 Mei 2019 - 09:24
Trump aongeza vikwazo zaidi kwa Iran

Rais wa Marekani Donald Trump ameongeza vikwazo kwa wananchi wa Iran huku amkiamini kwamba serikali ya Iran itakubali masharti ya Marekani.

ABNA: Rais wa Marekani Donald Trump ameongeza vikwazo kwa wananchi wa Iran huku amkiamini kwamba serikali ya Iran itakubali masharti ya Marekani.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ikulu ya Marekani, Trump alisema anatarajia viongozi wa Iran wampigie simu. Aidha rais huyo amesema kuwa aliamuru kupelekwa kundi la manowari zinazobeba ndege za kivita katika Ghuba ya Mashariki ya Kati kwa sababu ya vitisho vya Iran. Mwaka jana, Trump alijiondoa kutoka mkataba wa nyuklia na Iran na kisha akaongeza vikwazo dhidi ya nchi hiyo. Umoja wa Ulaya umetoa wito wa kuwepo suluhisho la kidiplomasia kwa mzozo huo. Hapo jana, viongozi wa jumuiya hiyo wakiongozwa na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel walisisitiza kuhusu dhamira yao ya kuuheshimu muafaka huo wa mwaka wa 2015, lakini wakasisitiza kuwa hawatakubali masharti yoyote.

Marekani imeendeleza kile inachokiita kuwa ni vikwazo vya hali ya juu dhidi ya Iran, ambapo Iran imeahidi kutosalimu amri kwa Marekani na kwamba haitakaa meza moja kujadiliana na Marekani.

Wakati huohuo Iran imetoa miezi miwili kwa mataifa ya Ulaya yaiunge mkono Iran au Iran ijitoe kwenye makubaliano hayo na kuendelea kurutubisha madini ya Uraniam kama zamani.

Mwisho wa habari/ 291